DRC: Mahakama ya Gombe kumsikiliza Vital Kamerhe kuhusu shutma zinazomkabili

Vital Kamerhe, mkurugenzi kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe, mkurugenzi kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi. REUTERS/Thomas Mukoya

Kesi ya aliyekuwa mnadhimu mkuu katika Ofisi ya rais jijini Kinshasa Vital Kamerhe inatarajiwa kurejelewa tena Jumatano Juni 3, 2020, kulingana na vyanzo vya mahakama.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya kifo cha mkuu wa mahakama ya mwanzo ya Gombe jijini Kinshasa, Raphael Yanyi, aliyefariki ghafla usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki iliyopita mjini Kinshasa.

Familia yake na mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini DRC yameomba mwili wa Raphael Yanyi ufanyiwe uchunguzi na vipimo mbalimbali ili kujua kwamba aliuawa au ni kifo cha kawaida.

Katika kesi ya hivi karibuni ambayo ilisikilizwa kwa dakika chache na baadaye kuahirishwa, Vital Kamerhe alikanusha madai ya kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa wakati kesi yake iliporejelewa Jumatatu Mei 25.

Akijibu baadhi ya maswali ya majaji kuhusu mikataba ya ununuzi wa nyumba kutoka kampuni ya Samibo inayomilikiwa na mfanyabiashara wa Lebanon, Samih Jamal, Vital Kamerhe alisema baadhi ya mikataba ilisainiwa bila ya yeye kupewa taarifa.

Kesi hii ya Vital Kamerhe na washtumiwa wenzake itasikilizwa kama vikao vikoa vingine vilivyotangulia katika jela kuu la Makala, jijini Kishasa.

Kesi hii inasikilizwa siku chache baada ya kifo cha mkuu wa mahakama ya mwanzo ya Gombe jijini Kinshasa, Raphael Yanyi, aliyefariki ghafla usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki iliyopita mjini Kinshasa.

Familia yake na mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini DRC yameomba mwili wa Raphael Yanyi ufanyiwe uchunguzi na vipimo mbalimbali ili kujua kwamba aliuawa au ni kifo cha kawaida.

Vital Kamerhe anashukiwa kwa kosa la ubadhirifu wa fedha za serikali ila wafuasi wa UNC wana matumaini na sheria ya DRC, licha ya kuwa wamekerwa kuona kiongozi kama huyo ametupwa jela badala ya kuwekwa chini ya ulinzi katika kizuizi cha nyumbani.

Kiongozi wa ofisi ya rais Felix Tshisekedi ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Muungano kwa Taifa la Kongo, UNC, anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za serikali zilizokuwa zimetengwa kwa maendeleo ya nchi, yaani mpango wa siku 100 wa rais.