DRC-BENI-MAUAJI-USALAMA

DRC: Kumi na nane wauawa katika shambulio jipya Djugu

Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mitaa ya eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri, unaoendelea kukumbwana machafuko ya kikabila, Machi 13, 2020.
Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mitaa ya eneo la Djugu, katika mkoa wa Ituri, unaoendelea kukumbwana machafuko ya kikabila, Machi 13, 2020. SAMIR TOUNSI / AFP

Watu 18 ikiwa ni pamoja na watoto walio na umri ulio chini ya miaka 6 wameuawa katika shambulio la hivi karibuni katika maeneo ya Mambisa wilayani DJUGU katika Mkoa wa ITURI Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mara nyingine kundi la wanamgambo wa Codeco wamehusishwa katika mauaji hayo mapya ya watu 18. Mkoa wa Ituri unaendelea kukumbwa na mauaji ya kikatili yanayodaiwa kutekelezwa na makundi ya watu wenye silaha; hasa kundi la wanamgambo la Codeco.

Baada ya shambulio hilo, askari wa jeshi la DRC, FARDC, waliwasili eneo la tukio na sasa wamùezindua operesheni kababambe ya kuwasaka waasi hao, amesema Alingi Adele, Mkuu wa wilaya ya Djugu.

"Watu waliouawa ni 16, ikiwa ni pamoja na wanaume 4, wanawake 7 na watoto 5, “ amesema Alingi Adele, huku akibaini kwamba wato walio uawa wana umri ulio chini ya miaka 5.

Mauaji ya raia yanayoshuhudiwa kila kukicha katika mkoa wa Ituri yameathiri vibaya hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani, amesema Innocent Madukadala, Mkuu wa eneo la Banyali Kilo.

"Idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka kwa kweli, wote wanakimbilia sehemu za Bunia, kwa sasa wamekosa hata msaada na una kuta kila familia ina watu 20 na hali hiyo inaleta tatizo sana katika masuala ya kibinadamu. Mashirika ya kihisani yameshindwa kuwafikia walengwa kutokana na hali hiyo ya wingi wa watu, " amesema Innocent Madukadala.

Serikali ya DRC inashtumiwa na wakazi wa Mkoa wa Ituri kwamba mapendekezo yao hayatiliwi maanani.

Kufikia sasa sio chini ya watu 32 ambao wameuawa katika kipindi cha siku nne mkoani Ituri.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu watu zaidi ya 300 wameuawa katika mkoa wa Iturina hali hiyo inawatia wasiwasi wanaharakati wa haki za binadamu katika mkoa huo.