DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Kesi ya Vital Kamerhe DRC: Mashahidi wasikilizwa

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. REUTERS/Baz Ratner

Kesi ya Vital Kamerhe kuhusu matumizi mabaya ya mali ya umma katika mpango wa dharura siku 100 wa rais Felix Tshisekedi, imerejelewa Jumatano wiki hii, wiki moja baada ya Raphael Yanyi, jaji aliyekuwa anafuatilia kesi hiyo kufariki dunia ghafla.

Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe na washtakiwa wengine wawili wanashtakiwa katika kesi ya madai ya kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa kama sehemu ya mpango wa siku 100 wa Félix Tshisekedi.

Kesi hii iliyosikilizwa kwa mara ya tatu Jumatano wiki hii ilisimamiwa na Jaji mkuu mpya wa mahakama: Jaji Pierrot Bankenge Mvita. Anachukuwa nafasi ya Raphaël Yanyi Ovungu, ambaye alifariki dunia ghafla wiki iliyopita.

Kwa mara ya kwanza Jumatano hii, mashahidi walisikilizwa katika kesi hiyo. Waziri wa zamani wa Maendeleo Vijijini Justin Bitakwira ni miongoni mwa mashahidi waliosikiliwza?

Justin Bitakwira ndiye ambaye alisaini mkataba wa awali mwaka 2018 na kampuni ya Samibo SARL ya mfanyabiashara wa Lebanon Samih Jammal, ambaye pia ni miongoni mwa washtakiwa.

Amebaini kwamba hapo awali ilikuwa mkataba wa karibu dola milioni 27 kwa ujenzi wa nyumba 900 zilizotengwa kwa mikoa 9 kote nchini.

Justin Bitakwira alikubali kuwa alitia saini kwenye mkataba huo. Lakini alibaini kwamba serikali haikuweza kulipa awamu ya kwanza ya malipo kwa kampuni ya Samibo SARL wakati huo. Aliongeza kuwa hakuweza kufuatilia suala hilo kwa sababu alikuwa ameondolewa na Vital Kamerhe kupitia barua rasmi. "Wakati Rais Félix Tshisekedi alichukuwa hatamu ya uongozi wa nchi, Kamerhe alizorotesgha serikali yetu. Tulifika tunakuwa kama watazamaji, "alisema mbele ya mahakama.

Amemshtumu mkurugenzi wa ofisi ya rais Felix Tshisekedi, na kuongeza kuwa hana taarifa kuhusu malipo ya dola milioni 57 kwa kampuni ya Samibo SARL. Kiwango hiki ni tofauti na kile cha dola milioni 27 katika mkataba wa awali.

"Sijawahi kusiani mkataba wowote wa DRC kulipa dola milioni 57. Yule ambaye alifanya hivyo aje akubali mwenyewe hapa, " alisema Justin Bitakwira.

Maneno haya yameungwa mkono na ushuhuda wa Ngongo Salumu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma, shahidi wa mwisho anatarajiwa kusikilizwa leo Alhamisi. Shahidi huyu pia amesema kwamba malipo hayo yalifanywa kwa msingi wa hati isiyo halali.