LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Serikali ya umoja wa kitaifa yatangaza kudhibiti kikamilifu mji wa Tripoli

Wapiganaji tiifu kwa Serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kuuweka tena kwenye himaya yao mji wa Tripoli, Juni 4, 2020.
Wapiganaji tiifu kwa Serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kuuweka tena kwenye himaya yao mji wa Tripoli, Juni 4, 2020. REUTERS/Ayman Al-Sahili

Wanajeshi wa serikali ya Libya, inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, wamefanikiwa kudhibiti kikamilifu jiji kuu la Tripoli kutoka mikononi mwa wanajeshi wa upinzani wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja mwaka mmoja baada ya jiji hilo kuwa mikononi mwa wanajeshi wa upinzani.

Msemaji wa jeshi hilo linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Mohammed Gnounou, amesema kwa sasa, jeshi linadhibiti maeneo yote ya jiji hilo, baada ya kuwarudisha nyuma, wapiganaji wa Jenerali Haftar.

Hata hivyo, jeshi la upinzani halijazungumzia suala hili lakini duru za kijeshi zinasema kuwa, wapiganaji wa upinzani wanajiaondoa katika Wilaya kadhaa z jiji la Tripoli.

Baada ya vikosi hivyo vya serikali kudhibiti tena jiji hilo, sasa vinadhibiti pia uwanja wa kimataifa wa ndege wa Tripoli ambao umefungwa tangu mwaka 2014.

Mapigano kati ya vikosi hivi pinzani, yalesababisha vifo vya mamia ya wanajeshi na watu wengine zaidi ya Laki Mbili kukimbia jiji hilo la Tripoli.

Haya yanajiri baada ya pande zote kukubali kurejelea mazugumzo ya amani, yaliyovunjika mapema mwaka huu.