DRC-UN-MAUAJI

UN: Watu 1,300 wauawa na makundi yenye silaha DRC

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Umoja wa Mataifa unasema watu karibu 1,300 wameuwa kutokana na mashambulizi ya raia yanayotekelezwa na makundi ya waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kusababisha  wengine zaidi ya Laki tano kukimbia makwao.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu katika Umoja huo Michelle Bachelet amesema visa vinavyoendelea kushuhudiwa nchini DRC ni uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Maeneo ambayo yameendelea kushuhudia visa hivyo katika siku za hivi karibuni ni katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.

Makundi ya waasi yanatuhumiwa kuhusika pakubwa kutekeleza mauaji hayo huku jeshi la serikali FARDC likituhumiwa pia kuhusika.

Katika mkoa wa Ituri, uchunguzi wa watalaam wa tume hiyo, umebaini kuwa, wanaotekeleza mashalbulizi dhidi ya rais ni waasi wa CODECO, kuanzia mwezi Machi mwaka huu baada ya kuaawa kwa kiongozi wake Ngudjolo Duduko Justin.

Katika Jimbo la Ituri peke yake kati ya mwezi Oktoba mwaka uliopita hadi mwezi Mei, raia 531 wameuawa huku 375 wakiuawa mwezi Machi pekee.

Tume hiyo inasema pamoja na mauaji hayo, visa vya ubakaji wa wanawake na wasichana pia vimekuwa vikitokea wakati raia wanapishambuliwa na kutaka serikali jijini Kinshasa kufanya vya kutosha kuwalinda raia.