Pata taarifa kuu
CAMEROON-VYOMBO VYA HABARI-USALAMA

Cameroon: Mwandishi wa habari Samuel Wazizi afariki dunia akiwa kizuizini

Mwandishi wa habari Samuel Wazizi alikufa akiwa kizuizini.
Mwandishi wa habari Samuel Wazizi alikufa akiwa kizuizini. RSF
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Jeshi la Cameroon limethibitisha kifo cha Samuel Wazizi, mwanahabari kutokja maeneo yanayozungumza Kiingereza aliyefariki dunia akiwa kizuizini.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii ya kifo cha Samuel Wazizi kilitolewa na mashirika ya kiraia Jumatano wiki hii, huku yakilaani vitendo vya kikatili alivyofanyiwa akiwa kizuizini, baaada ya kushtumiwa na serikali kuwa "anashirikiana na magaidi", kulingana na taarifa ya mashirika hayo.

Taarifa iliyotiliwa saini na mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Wizara ya Ulinzi imethibitisha kifo cha mwandishi huyo wa habari na kukata kitumani kwa wale ambao walikuwa na imani kuwa bado yuko hai. Samuel Wazizi alifariki dunia, taarifa hiyo ilimalizia.

Kuhusu mazingira ya kifo chake, taarifa ya wizara ya Ulinzi inabainisha kuwa baada ya kukamatwa Agosti 2 huko Ekona, Kusini-magharibi mwa nchi, Samuel Wazizi ambaye jeshi linamtaja kama "mweka hazina wa makundi mbali mbali ya kigaidi" alikuwa amepelekwa kuhojiwa na idara husika huko Yaoundé. Hata hivyo alipokelewa kwenye idara hiyo akiwa katika hali mbaya ya kiafya na hivyo kupelekwa hospitalini mara moja. Lakini alifariki dunia siku chache baadaye, Agosti 17, 2019 , kutokana na mchuko. Hajafanyiwa kitendo chochote kile cha kikatili au mateso ya aina yoyote, amebaini mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Wizara ya Ulinzi.

Chama cha waandishi wa habari nchini Cameroon, SNJC, na Chama cha waandishi wa habari kutoka maeneo yanayozungumza Kiingereza nchini humo yamefutilia mbali maelezo hayo ya Wizara ya Ulinzi, na kusema kuwa ni uongo mtupu.

Denis Nkwebo, kiongozi wa chama cha waandishi wa habari nchini Cameroon, SNJC amesema maelezo hayo ya wizara ya ulinzi ni ya kejeli kwa familia ya Samuel Wazizi na waandishi wa habari nchi Cameroon kwa ujumla.

Wakati huo huo muungano wa vyama vya waandishi wa habari katika maeneo yanayozungumza Kiingereza umeitisha maandamano leo Jumamosi Juni 6 katika mji wa Yaounde.

Denis Nkwebo amesema kuwa maelezo ya serikali yamejaa uongo, akianzia tu ktangu mwandishi huyo alikamatwa.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, shirika la Waandishi wa Habari wasiokuwana Mipaka, RSF, limesema limeghadhibishwa na maelezo ya Wizara ya Ulinzikuhusu kifo cha mwandishi wa habari Samuel Wazizi Agosti 17, 2019. RSF imebaini kwamba haijulishwa kamwe kuhusu kifo chake na mwandishi huyo wa habari alikuwa katika hali nzuri ya afya wakati alipokamatwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.