DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Hatma ya Vital Kamerhe kujulikana Juni 20

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. REUTERS/Baz Ratner

Mnadhimu wa zamani wa Ofisi ya rais wa DRC, Vital Kamerhe, anakabiliwa na kifungo cha miaka 20, baada ya kesi hiyo kumalizika jana katika gereza  kuu la Makala jijini Kinshasa, mji mkuu wa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Wakati kesi hiyo ilikuwa ikisikiliwza Alhamisi wiki hii, mwendesha mashitaka aliomba kifungo cha miaka 20 dhidi ya Vitral Kamerhe. Hata hivyo wanasheria wake wameomba mteja wao aachiliwe huru, wakibaini kwamba hana hatia yoyote.

Upande wa mashtaka unataka  Kamerhe ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela, pamoja na kunyang'anywa mali zake anazodaiwa kuwa zilipatikana kwa fedha za umma.

Hata hivyo, Mashirika ya kiraia yameonyesha kuwa hayajafurahishwa na namna ambavyo kesi hiyo imekuwa ikiendeshwa.

Bw. Kamerhe na washtakiwa wengine wawili kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa.