Vikosi vya Burkina Faso vyaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wa Katiba Macina
Imechapishwa:
Majeshi ya Burkina Faso yanaendelea na operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Kislamu wa kundi la Katiba Macina katika msitu unaopatikana kwene eneo la mpakani na nchi jirani ya Burkina Faso.
Kwa miezi kadhaa, vikosi vya kupambana na ugaidi vya Burkina Faso vimekuwa vikiwasaka wanamgambo wa kundi la Katiba Macina ambao wanatafuta kujidhatiti katika eneo hilo.
Katika upande wa Burkina Faso, vikosi vya kupambana na ugaidi bado vipo, msituni, kuyasaka makundi ya watu wenye silaha ambao hivi karibuni walifanya shambulio dhidi ya kituo cha askari wa Côte d’Ivoire.
Kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa jeshi la Burkina Faso, operesheni hiyo ilianza muda mrefu kabla ya operesheni ya pamoja. "Vikosi vyetu maalum bado vinaendelea kuwasaka wauaji ," kilisema chanzo hicho.
Lengo ni kupata na kuvunja ngome mbali mbali za makundi ya kigaidi yanayopiga kambi katika misitu hii. Kulingana na vyanzo vyetu, magaidi hao wameweka ngome kadhaa katika misitu hii, pande zote mbili za mpakani.
Kufuatia Operesheni "Comoé", watu hawa wenye silaha wametawanyika katika misitu hii, pande zote mbili za mpakani. Makundi haya yenye silaha yana mtandao mkubwa wa mawasiliano katika sehemu hizi tofauti za msitu wanazodhibiti, baadhi ya vyanzo vimebaini.
"Hata kama tumeweza kuua baadhi yao wakati wa Operesheni Comoé, bado makundi haya yana nguvu katika eneo hili," kimesema chanzo kingine cha usalama.
Kulingana na mtafiti Mahamoudou Sawadogo, opresheni hii itakuwa ngumu sana kama Ghana haitashiriki.
Ghana inachangia sehemu ya eneo hili la misitu na Burkina Faso na Côte d'Ivoire.