SOMALIA-SOMALILAND-USHIRIKIANO

Somalia na Somaliland wafanya mkutano wa kihistoria

Muse Bihi Abdi, rais wa Somaliland, Novemba 13, 2017 huko Hargeisa. (Picha kumbukumbu)
Muse Bihi Abdi, rais wa Somaliland, Novemba 13, 2017 huko Hargeisa. (Picha kumbukumbu) AFP

Marais wa Somalia na mkoa wa zamani wa Somalia uliojitenga wa Somaliland mwaka 1991, wamekutanauso ana kwa ana kwa mara ya kwanza Jumapili hii Juni 14 katika mji mkuu wa Djibouti.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa pande hizo mbili ulifanyika huko Djibouti na ulisimamiwa na rais wa Djibouti Ismail Imar Guelleh na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Huu ni "mkutano wa mashauriano" wenye lengo la kuanzisha mazungumzo kufuatia mgogoro uliozuka kati ya miji hiyo mikuu miwili.

Wakati huo huo Serikali ya Somalia, imemtambua rasmi kiongozi mwenye utata wa jimbo lenye mamlaka yake ya ndani ya Jubaland, Ahmed Madobe, baada ya miezi kadhaa ya mvutano.

Ahmed Madobe ambaye ni mbabe wa zamani wa kivita alichaguliwa tena kama rais wa jimbo hilo mwezi Agosti 2019, katika uchaguzi ambao serikali kuu ilisusia.

Hata hivyo Serikali ya Somalia imesema uongozi wa mpito wa Madobe utadumu kwa miaka miwili, tofauti na muhula wa miaka minne kulingana na katiba ya Jubaland.

Juhudi za maridhiano kati ya Somalia na Somaliland hazijazaa matunda yoyote mpaka sasa.