MALI-ALGERIA-AQMI-USALAMA

Sahel: AQMI yathibitisha kifo cha kiongozi wake Droukdel

Abdelmalek Droukdel, kiongozi wa kundi la AQMI, mwaka 2010.
Abdelmalek Droukdel, kiongozi wa kundi la AQMI, mwaka 2010. AFP/THOMAS COEX

Kundi la AQMI lenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda limethibitisha katika video, kifo cha kiongozi wake, Abdelmalek Droukdel, kilichotangazwa na Ufaransa mwanzoni mwa mwezi Juni, kulingana na tovuti ya shirika la Marekani linalochunguza makundi ya kijihadi.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo AQMI imeahidi kuendelea na vita dhidi ya majeshi ya Ufaransa na majeshi mengine yalioko Afrika Kaskazini na ukanda wa Sahel, amesema Mkurugenzi wa shirika hilo Rita Katz, kwenye ukurasa wake wa.

Mapema mwanzoni mwa mwezi Juni Ufaransa ilitangaza kwamba vikosi vyake maalum vilimuangamiza Abdelmalek Droukdel kaskazini mwa Mali, kwenye mpaka na Algeria.

Wakati huo huo Marekani imesema ilisaidi kutoa taarifa na msaada kwa kumuangamiza kiongozi huyo wa kundi la AQMI.