DUNIA-WAKIMBIZI-VITA-MAJANGA YA ASILI-USALAMA

Siku ya wakimbizi duniani yaadhimishwa

Mtaa wa kibiashara katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
Mtaa wa kibiashara katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Sally Hayden/SOPA Images/LightRocket via Getty Images

Leo dunia inaadhimisha siku ya wakimbizi, wakati huu dunia inapoendelea kupambana na janga hatari la Corona, ambalo limesababisha vifo vingi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Mamilioni ya watu wameendelea kufungasha virago kila uchao kwenda kusaka usalama wakikimbia vita, mateso, mauaji, njaa na sambabu zingine mbalimbali. Japo wakimbizi hawa wanaonekana mzingo machoni mwa wengi, Umoja wa Mataifa unasema dunia ikiwakumbatia itaoona mchango wao na faida yao.

Watu zaidi ya Milioni 80, hasa wanawake na watoto pamoja na wanaume wameyakimbia makwao kwa sababu ya vita na majanga mengine.

Wakuu wa Umoja wa Mataifa wanahofia kuwa huenda janga la Corona likawaathiri zaidi wakimbizi ambao wanaishi katika kambi za wakimbizi kote duniani.

Mkuu wa Tume ya kuwahudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, ametoa wito kwa dunia kuwakumbuka wakimbizi katika kipindi hiki kigumu.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake wa siku ya wakimbizi duniani ameeleza ahadi ya Umoja wa Mataifa kukomesha migogoro na mateso yanayosababisha mamilioni ya watu kuwa wakimbizi.