LIBYA-UFARANSA-UTURUKI-USALAMA

Emmanuel Macron: Uturuki inacheza 'mchezo hatari' nchini Libya

Emmanuel Macron wakati wa mkutano wake wa pamoja wa waandishi wa habari na rais wa Tunisia Kaïs Saïed, Juni 22 huko ikulu ya Elysée.
Emmanuel Macron wakati wa mkutano wake wa pamoja wa waandishi wa habari na rais wa Tunisia Kaïs Saïed, Juni 22 huko ikulu ya Elysée. Christophe Petit Tesson/Pool via REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Uturuki inacheza 'mchezo hatari' nchini Libya, katika kile alichoeleza ni tishio la moja kwa moja kwa bara nzima la Ulaya na haitaruhu nchi hiyo kuendelea kuingilia nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.

Matangazo ya kibiashara

Rais Macron ameitoa Kauli hiyo wakati alipokutana na mwenzake wa Tunisia Kaïs Saïed, jijini Paris.

Hivi karibuni, msemaji wa ikulu ya rais wa Uturuki alisema usitishwaji wa mapigano huko Libya utatekelezwa kwa sharti kuwa wapiganaji wanaojiita Jeshi la Taifa la Libya wanaoongozwa na Jenerali muasi Khalifa Haftar waondoke katika mji wa Sirte.

Hivi karibuni rais wa Misri alitishia kuingilia kijeshi nchini Libya, kauli ambayo serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoliinayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa ililaani na kusema kuwa iko tayari kujibu mashambulizio yoyote kutoka nje ya mipaka ya Libya.

Kauli ya Abdel Fattah Al-Sisi imeungwa mkono na Ufaransa na kubaini kwamba Misri ina haki ya kulinda vilivyo usalama wake.

Mataifa ya Magharibi yameendelea kugawanyika kuhusu mzozo unaoendelea nchini Libya.