LIBYA-AMANi-USALAMA-SIASA

Umoja wa nchi za Kiarabu waunga mkono Cairo kuhusu amani Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Ahmed Abul Gheit mbele ya Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa nchi za umoja huo Juni 23, 2020 huko Cairo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Ahmed Abul Gheit mbele ya Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa nchi za umoja huo Juni 23, 2020 huko Cairo. murad FATHI / Arab League / AFP

Mataifa yanayounda Umoja wa Kiarabu yametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuacha kuingilia kati masuala ya Libya, na kutaka pia kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa nchi za Kiarabu umeunga mkono msimamo wa Misri wa kutaka kuvunjwa kwa wanamgambo na kuowaondoa mamluki nchini Libya na hivyo kurahisishia mkataba wa kusitisha mapiganouliofikiwa hivi karibuni kati ya pande hasimu nchini humo.

Katika taarifa yao ya mwisho, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Umja wa Kiarabu wametoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja nchini Libya, na hasa kupunguza uhasama karibu na mji wa Sirte, hali ambayo itawezesha haraka kuanza tena kwa mazungumzo chini ya mwavuli wa Umoja aw Mataifa.

Pia wamesema wanaunga mkono mchakato wa kipekee wa kisiasa, mbali na suluhisho lolote la kijeshi, na kuomba jumuiya ya kimataifa kuacha kuingilia kati masuala ya nchi za Kiarabu, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu nchi zilizoingilia kijeshi nchini Libya.

Wito huu unakuja baada ya rais wa Ufaransa Emmanuel  Macron kukutana na kufanya mazungumzo na rais mwenzake wa Tunisia mjini Paris, Kais Saied.

Rais Saied  anasema  nafasi ya Uturuki nchini Libya inahatarisha maslahi ya nchi hiyo, majirani zake,na bara la Ulaya.