MALAWI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Raia wa Malawi waombwa kuwa watulivu kwa kusubiri matokeo ya uchaguzi

Wananchi wa Malawi wanasubiri matokeo ya mwisho kutoka kwa Tume ya Uchaguzi, huku ushindani ukisalia kati ya kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera na rais Peter Mutharika.
Wananchi wa Malawi wanasubiri matokeo ya mwisho kutoka kwa Tume ya Uchaguzi, huku ushindani ukisalia kati ya kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera na rais Peter Mutharika. MBC

Vyombo vya Habari nchini Malawi vinaripoti kuwa kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera anaongoza kwa kura dhidi ya rais Peter Mutharika, wakati huu wananchi wa taifa hilo wakisubiri matokeo baada ya kuoiga kura siku ya Jumanne.

Matangazo ya kibiashara

Matokeo yasiyo rasmi yanayotangazwa na vyombo hivyo vya Habari, yanaonesha kuwa Chakwera anaongoza kwa asilimia 55 baada ya robo tatu ya kura zote kuhesabiwa huku rais Mutharika akiwa na asilimia 40.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Chifundo Kachale, ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuwa watulivu wakati huu maafisa wa tume hiyo wanapoendelea kujumuisha matokeo kabla ya kumtangaza mshindi.

Aidha, ameongeza kuwa ujumuishaji wa matokeo unafanyika kwa njia ya kawaida na kuwataka wananchi kutoamini ripoti wanazoziona kwenye mitandao ya kijamii.

Wapiga kura nchini humo walipiga kura tena baada ya Mahakama mwezi Februari kufuta ushindi wa rais Mutharika baada ya ushahidi wa wizi wa kura na kuifanya nchi hiyo kuwa ya pili baada ya Kenya, kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais.

Kwa sasa, wananchi wa Malawi wanasubiri matokeo ya mwisho kutoka kwa Tume ya Uchaguzi, huku ushindani ukisalia kati ya kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera na rais Peter Mutharika.