DRC-WHO-EBOLA-AFYA

DRC na WHO zatangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola Mashariki mwa nchi

Watu 2,277 ndio walifariki dunia kutokana na Ebola, na watu elfu 1,171 ndio walipona homa hiyo hatari, baada ya kuambukizwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo katika eneo hili la Mashariki mwa DRC mwaka wa 2018.
Watu 2,277 ndio walifariki dunia kutokana na Ebola, na watu elfu 1,171 ndio walipona homa hiyo hatari, baada ya kuambukizwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo katika eneo hili la Mashariki mwa DRC mwaka wa 2018. REUTERS/Goran Tomasevic/File Photo

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikishirikiana na Shirika la Afya Duniani, WHO, imetangaza rasmi kumalizika kwa ugonjwa wa Ebola katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Afya Eteni Longondo amesema ugonjwa huo, ambao ulidumu kwa muda mrefu zaidi tangu Agosti mwaka 2018 umesababisha vifo vya watu zaidi ya 2.000, pia amepongeza ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya Ebola.

Hata hivyo serikali ya DRC imewataka wananchi kuendelea kuwa makini, kufuatia magonjwa mengine yanayoendelea kulikumba taifa hilo.

Watu 2,277 walifariki dunia kutokana na Ebola, na watu elfu 1,171 ndio walipona homa hiyo hatari, baada ya kuambukizwa, tangu kuzuka kwa ugonjwa huo katika eneo hili la Mashariki mwaka wa 2018.

Mbali na ugonjwa aw Ebola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na kitisho kingine ugonjwa hatari wa Covid-19 unaosumbua ulimwengu.

Kufikia sasa DRC imerekodi visa 6,411 vya maambukizi ya Corona, ugonjwa ambao umeuwa watu 142 baada ya vifo vipya 7 kuthibitishwa. Wagonjwa 885 wamepona ugonjwa huo.