SUDAN-UCHUMI

Nchi zaidi ya arobaini zaichangia Sudan dola Bilioni mbili

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok. Ebrahim HAMID / AFP

Jumuiya ya Kimataifa imeichangia Sudan dola bilioni Bilioni mbili kusaidia nchi hiyo kuinua uchumi wake unaoendelea kudorora tangu kuanguka kwa utawala wa rais Omar al-Bashir.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo wa ushirikiano, ulioandaliwa na Jumuiya ya Ulaya, Umoja wa Mataifa, Ujerumani na Sudani, ulifanyika Alhamisi Juni 25 alasiri. Lengo ilikuwa kutoa mchango wa dola bilioni Bilioni mbili, kwa kuisaidia Sudan, nchi inayokabiliwa na kitisho cha mdororo mkubwa wa uchumi.

Nchi hizo zimeahidi kuchangia dola Bilioni mbili kuwezesha utekelezaji wa mpango mkubwa wa mageuzi ya kiuchumi uliopendekezwa na Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok.

“Ni muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa kifedha kwa taifa hilo linajikongoja ili kuenzi mageuzi ya kidemokrasia yaliyopatikana pamoja na kuhakikisha utulivu nchini Sudan, “ amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Hata hivyo kiwango kilichotolewa na mkutano huo ni kidogo ikilinganishwa na ombi la dola bilioni 8 lililotolewa na serikali ya Sudan ili kunusuru uchumi wa taifa hilo unaoandamwa na ukosefu wa ajira na athari za janga la virusi vya corona.

Mataifa yaliyoichangia fedha nchi hiyo ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Muungano wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia pamoja na taasisi za kikanda ikiwemo Umoja wa Ulaya na mashirika ya fdha ya kimataifa

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok ameshukuru na kusifu jitihada hiyo ya kuipiga jeki nchi yake ambayo inapitia kipindi kigumu cha mpito chini ya serikali ya mseto kati ya raia na majenerali wa jeshi.