NIGER-USALAMA

Visa vya utekaji nyara vyakithiri Niger

Askari wa Nige huko Niamey, le 7 juillet 2019.
Askari wa Nige huko Niamey, le 7 juillet 2019. ISSOUF SANOGO / AFP

Maafisa wa usalama nchini Niger wamethibitisha kuwa Wafanyakazi kumi wa shirika la misaada ya Chakula waliotekwa nyara siku ya Jumatano na kundi la wanajihadi katika eneo la kusini magharibi mwa Niger, karibu na Burkina Faso, wanaendelea kushikiliwa katika eneo lisilojulikana.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo la misaada APIS, linaloshirikiana na shirika la kimataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Kadidiatou Harouna, wafanyakazi hao kumi walitekwa nyara siky ya Jumatano wiki iliyopita wakati wakisambaza chakula katika kijiji kimoja kilichoko kwenye eneo la Kusini Magharibi mwa Niger, karibu na Burkina Faso.

Harouna ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa mashuhuda waliwaona wapiganaji wakijihadi  wenye silaha na pikipiki ambao waliingia katika kijiji hicho wakati shughuli ya kugawa chakula ikiendelea na kuwataka wafanyakazi hao wawafuate mara moja.

Hii sio mara ya kwanza vitendo vya utekaji kushuhudiwa katika eneo hilo. Mara ya mwisho mfanyakazi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali, raia wa Ujerumani, na padre mmoja kutoka Italia walitekwa nyara mwaka wa 2018 katika mkoa ulioko eneo la mpka kati ya Niger, Burkina Faso na Mali, eneo ambalo limekuwa maficho ya wapiganaji wa kijihadi huko Sahel.