SUDAN-LIBYA-USALAMA

Mamluki 122 wakamatwa Darfur

Serikali ya Sudan imetangaza kwamba inawashikilia mamluki 122 waliokamatwa katika Jimbo la Darfur wakijaribu kwenda nchini Libya kushiriki vita vinavyoendelea nchini humo.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdock huko Khartoum Desemba 11, 2019.
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdock huko Khartoum Desemba 11, 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi hili la wapiganaji, wakiwemo watoto wanane, walikuwa wakisafiri kwenda Libya ili kushiriki vita vinavyoendelea nchini humo.

Ikiwa, kulingana na ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa, mamia au hata maelfu ya raia wa Sudan wanashiriki vita mara kwa mara nchini Libya, hii ni mara ya kwanza Khartoum kutangaza rasmi kuwakamata raia wake wanoshiriki vita nchini humo.

Katika video iliyotolewa na shirika la habari la serikali, Suna, vijana kadhaa wanaonekana wamekaa sakafuni wakizungukwa na vikosi vya usalama.

Picha hizo, zilizotengenezwa katika mji wa El Geneina, mji mkuu wa jimbo la magharibi mwa Darfur, kwenye mpaka na Chad na Libya, zinaonyesha wapiganaji ambao walikuwa wakijiandaa kuingia katika nchi jirani, mamlaka nchini Sudan imesema.

Sudan mara kadhaa ilikuwa ikinyooshewa kidole kuhusika na machafuko nchini Libya. Serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli ilikuwa inashutumu vyama vya Sudan kwa kutuma wapiganaji kusaidia kambi ya mpinzani wake, Marshal Khalifa Haftar, madai ambayo serikali ya Sudan wameendelea kukanusha.

Sudan mara kadhaa ilikuwa ikinyooshewa kidole kuhusika na machafuko nchini Libya. Serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli ilikuwa inashutumu vyama vya Sudan kwa kutuma wapiganaji kusaidia kambi ya mpinzani wake, Marshal Khalifa Haftar, madai ambayo serikali ya Sudan wameendelea kukanusha.

Katika ripoti yake ya mwezi Desemba 2019, Umoja wa Mataifa ulithibitisha uwepo wa wapiganaji wa Sudan wakisaidia kambi ya Marshal Khalifa Haftar lakini pia na kambi ya serikali ya Tripoli.