Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Serikali ya DRC yakumbwa na mvutano mkubwa

Rais wa DRC Félix Tshisékédi na mtangulizi wake Joseph Kabila wakati wa hafla ya kuapishwa kwake huko Kinshasa, Januari 24, 2019.
Rais wa DRC Félix Tshisékédi na mtangulizi wake Joseph Kabila wakati wa hafla ya kuapishwa kwake huko Kinshasa, Januari 24, 2019. REUTERS/Olivia Acland
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukumbwa na malumbano ya ndani baada ya mtafaruku kati ya vigogo kutoka pande mbili zilizoko madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Hakuna kinachoendelea kati ya pande mbili zilizoko madarakani, muungano wa vyama wa FCC unaoongozwa na Joseph Kabila, na muungano wa CACH wa Félix Tshisekedi, bali ni mvutano mtupu, hali ambayo imezua mkanganyiko katika nchi hiyo kubwa katika Ukanda wa Afrika ya Kati.

"Kisingizio cha mzozo huu mpya, wanasema wadadisi, ni mapendekezo matatu yaliyoletwa na wabunge wawili kutoka chama cha FCC, Sakata na Minaku. Mapendekezo ya muswada wa sheria kuhusu mageuzi ya vyombo vya sheria ambayo hayakuungwa mkono na wengi. Wanashuku kwa baadhi ya mapendekezo yaliyotetewa na wabunge hao wawili, nia ya kurasimisha mfumo wa mahakama kwa serikali kwa ujumla na kwa Waziri wa Sheria upande mwingine.

Lakini kilichosababisha mgogoro huo, Ledjely, mmoja wa wadadisi hao kutoka Guinea akihojiwa na RFI amesema, ni hatua ya Waziri wa Sheria kuwasilisha mtazamo wa serikali unaohusiana na mapendekezo haya matatu kwa Bunge, bila kumhusisha rais Félix Tshisekedi au serikali. Tabia ambayo rais Tshisekedi anafasiri kama kudharau mamlaka yake. Kitendo ambacho kilimkasirisha hadi kuchukuwa uamuzi wa kusitisha ghafla ushiriki wake katika kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho alikuwa anaongoza siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Siku iliyofuata mambo yalishika kasi baada ya kukamatwa Célestin Tunda Ya Kasende, naibu waziri mkuu anayesimamia haki. Chini ya shinikizo, mwendesha mashtaka aliamua kumuachilia waziri huyo baada ya mahojiano ya muda mfupi, amesema Ledjely.

Hali hii imeendelea kuzua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tayari pande hizo mbili zimeendelea kuzusha sintofahu nchini humo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.