UFARANSA-G5 SAHEL-USALAMA

Emmanuel Macron ashiriki mkutano wa kilele wa G5 Sahel nchini Mauritania

Askari wa kikosi cha Ufaransa, Barkhane, wakati wa operesheni iliyowezesha kuuawa kwa kiongozi mkuu wa AQIM Abdelmalek Droukdel katika eneo la Sahel, Kaskazini mwa Mali. (Picha ya tarehe 11 Juni, 2020).
Askari wa kikosi cha Ufaransa, Barkhane, wakati wa operesheni iliyowezesha kuuawa kwa kiongozi mkuu wa AQIM Abdelmalek Droukdel katika eneo la Sahel, Kaskazini mwa Mali. (Picha ya tarehe 11 Juni, 2020). defense.gouv.fr/operations

Viongozi wa G5 Sahel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wanakutana Jumanne hii, Juni 30, kwa mkutano wa kilele huko Nouakchott, nchini Mauritania.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza nje ya Ulaya ya Emmanuel Macron tangu kuzuka kwa ugonjwa hatari wa Covid-19, "ishara ya mpya ya mshikamano", kulingana na ikulu ya Élysée.

Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika na Louise Mushikiwabo katibu mkuu wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) na Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, pia watashiriki mkutano huo.

Viongozi wa Italia na Ujerumani pia watapewa nafasi kushiriki mkutano huo kupitia video. Viongozi hao wanatarajia kujadili mkakati uliozinduliwa karibu miezi sita iliyopita katika mkutano wa mwisho huko Pau, Kusini Magharibi mwa Ufaransa. Kipindi ambacho, kwa mtazamo wa Ufaransa, kilikuwa kizuri kwa kikosi cha nchi hiyo katika Ukanda wa Sahel, Barkhane.

Vikosi vya kimataifa kutoka nchi tano katika ukanda aw Sahela vikisaidiwa na vikosi vya Ufaransa, Barkhane, wameendelea kutokomeza makundi yenye silaha yanayohatarisha usalama katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic State katika eneo la Sahara (EIGS).

Hayo yanajiri wakati Bukrkina Faso inaingia kipindi kigumu cha uchaguzi ambacho kinatia wasiwasi Ufaransa.

Tume ya Umoa wa Mataifa pamoja na mahirika yasiyo ya kiserikali yameendelea kushutmu vikosi vya serikali za Mali , Niger na Burkina Faso kuhusika na baadhi ya vitendo vya kikatili kama vile mauaji dhidi ya raia.