UBELGIJI-DRC-USHIRIKIANO-SIASA-USALAMA

Mfalme wa Ubelgiji: 'Ninasikitishwa' na dhulma za enzi za ukoloni DRC

Bendera mpya ya Jamhuri ya Congo, Julai 1, 1960, siku ambayo Congo (DRC) ilipata rasmi uhuru kutoka Ubelgiji.
Bendera mpya ya Jamhuri ya Congo, Julai 1, 1960, siku ambayo Congo (DRC) ilipata rasmi uhuru kutoka Ubelgiji. Bettmann / Getty Images

Mfalme wa Ubelgiji Philippe ameelezea masikitiko yake, leo Jumanne Juni 30, kwa mara ya kwanza katika historia ya Ubelgiji, " kwa majeraha" yaliyosababishwa wakati wa ukoloni wa Ubelgiji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua iliyotumwa Jumanne kwa rais wa DRC, Félix Tshisekedi, wakati DRC inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wa wake, Mfalme Philippe ameandika: "Nataka kuelezea masikitiko yangu makubwa kwa majeraha haya ya zamani, ambayo maumivu bado yanaendelea hadi leo kutokana na ubaguzi ambao bado upo katika jamii zetu ”.

"Wakati wa taifa huru la Congo (wakati eneo hili la Kiafrika lilikuwa chini ya utawala wa mfalme wa zamani Léopold II) vitendo vya ukatili na vya aibu vilitekelezwa, na ambavyo bado vinaendelea kusababisha maumivu makubwa katika nyoyo zetu" , amebaini Mfalme Philippe, ambaye ameongeza kuwa "kipindi cha ukoloni ambacho kilifuata (kile Congo-Belge kuanzia mwaka 1908 hadi mwaka 1960) pia kilisababisha mateso na aibu".

Kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd, aliyefariki dunia mikononi mwa polisi mwishoni mwa Mei huko Minneapolis, kiliibuka hisia tofauti kote ulimwenguni na pia nchini Ubelgiji, mjadala kuhusu ghasia za kipindi cha ukoloni nchini DRC na jukumu lenye utata la hayati Mfalme Leopold II ambaye anatuhumiwa na wanaharakati wengine wanaopiga vita ukoloni kuwa aliwauwa mamilioni ya raia wa Congo.

Sanamu ya Leopold II iliyopakwa rangi nyekundu huko Antwerp, Ubelgiji, Juni 4, 2020.
Sanamu ya Leopold II iliyopakwa rangi nyekundu huko Antwerp, Ubelgiji, Juni 4, 2020. JONAS ROOSENS / BELGA / AFP

Katika muktadha huu, Mfalme Philippe amejikubalisha "kupambana na kila aina ya ubaguzi wa rangi". "Ninakaribisha hatua ya bunge letu ambalo limeanzisha mchakato wa kukumbuka masaibu yaliyotokea katika mataifa yaliyokuwa chini ya utawala wetu katika enzi za ukoloni na kuweza kuomba msamaha", ameongeza Mfalme wa Ubelgiji katika barua yake.

Maneno haya ya Mfalme wa Ubelgiji yanakuja wakati sintofahamu inaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokana na mgogoro wa kisiasa uliochochewa na tukio ha hivi karibuni la kukamatwa kwa naibu Waziri mkuu anayeshusika na masuala ya sheria nchini humo naibu waziri mkuu anayesimamia haki, Celestin Tunda Ya Kasende.

Kwa takribani wiki moja sasa, wafuasi wa chama cha UDPS kinachoongozwa na rais Felix Thisesekedi, wamekuwa wakiandamana kupinga muswada uliowasilishwa na wabunge wa FCC wanaotaka kumpa madaraka makubwa naibu waziri mkuu anayesimamia haki, Celestin Tunda Ya Kasende.

"Kisingizio cha mzozo huu mpya, wanasema wadadisi, ni mapendekezo matatu yaliyoletwa na wabunge wawili kutoka chama cha FCC, Sakata na Minaku. Mapendekezo ya muswada wa sheria kuhusu mageuzi ya vyombo vya sheria ambayo hayakuungwa mkono na wengi. Wanashuku kwa baadhi ya mapendekezo yaliyotetewa na wabunge hao wawili, nia ya kurasimisha mfumo wa mahakama kwa serikali kwa ujumla na kwa Waziri wa Sheria upande mwingine.

Lakini kilichosababisha mgogoro huo, Ledjely, mmoja wa wadadisi hao kutoka Guinea akihojiwa na RFI amesema, ni hatua ya Waziri wa Sheria kuwasilisha mtazamo wa serikali unaohusiana na mapendekezo haya matatu kwa Bunge, bila kumhusisha rais Félix Tshisekedi au serikali. Tabia ambayo rais Tshisekedi anafasiri kama kudharau mamlaka yake. Kitendo ambacho kilimkasirisha hadi kuchukuwa uamuzi wa kusitisha ghafla ushiriki wake katika kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho alikuwa anaongoza siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Hali hii imeendelea kuzua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tayari pande hizo mbili zimeendelea kuzusha sintofahu nchini humo.