UN-USALAMA

Coronavirus: Umoja wa Mataifa waomba kusitishwa kwa migogoro

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloomba kumaliza migogoro duniani ili kuwezesha vita dhidi ya janga la Covid-19, baada ya zaidi ya miezi mitatu ya mazungumzo.

Azimio hilo linalenga kuunga mkono wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Machi 23 wa kusitisha mapigano duniani.
Azimio hilo linalenga kuunga mkono wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Machi 23 wa kusitisha mapigano duniani. Johannes EISELE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo, lililopitishwa katika kura iliyoandikwa, liliandaliwa na Ufaransa na Tunisia, ambazo zimekaribisha kupitishwa kwake, huku balozi wa Tunisia kwenye Umoja aw Mataifa, Kais Kabtani, akibaini kwamba ni "mafanikio ya kihistoria" kwa nchi hizo mbili.

Wataalam wengine wana mashaka ya hali itakayotokea baadaye kuhusu azimio hilo baada ya shughuli za baraza hilo kuzorota kwa muda mrefu.

Azimio hilo linalenga kuunga mkono wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Machi 23 wa kusitisha mapigano duniani.

Azimio hilo linataka "kusitishwa mapigano haraka na kwa jumla" katika mizozo yote iliyowekwa kwenye ajenda ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, isipokuwa vita dhidi ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu.