ETHIOPIA-USALAMA

Hamsini wauawa katika makabiliano Ethiopia

Kiongozi wa wa upinzani Jawar Mohammed kutoka jamii ya Oromo (katika shati la rangi nyeupe) anatembea akizungukwa na polisi, Oktoba 23, 2019, huko Addis Ababa, Ethiopia.
Kiongozi wa wa upinzani Jawar Mohammed kutoka jamii ya Oromo (katika shati la rangi nyeupe) anatembea akizungukwa na polisi, Oktoba 23, 2019, huko Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Tiksa Negeri

Watu Hamsini waliuawa jana wakati wa maandamano katika jimbo la Oromiya nchini Ethiopia baada ya makabiliano na polisi, walipokuwa wanalaani kuuawa kwa mwanamuziki mashuhuri Hachalu Hundessa aliyepigwa risasi siku ya Jumatatu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa vyombo vya usalama nchini humo Getachew Balcha amesema maafisa wa usalama ni miongoni mwa watu waliouawa katika maandamano hayo yaliyofanyika pia katika jiji kuu Addis Ababa.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa mauaji haya yamechewa kisiasa hasa baada ya kuuawa kwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa.

Katika hatua nyingine, Jawar Mohammed kiongozi maarufu wa upinzani kutoka la Oromiya ambalo pia ndilo analotokea Waziri Mkuu, Abiy Ahmed,amekamatwa na walinzi wake na mmoja wa viongozi wa chama chake, Bekele Gerba baada ya kukataa kusalimisha silaha yake.