Macron: Ulaya na G5 Sahel watendeleza mapambano dhidi ya ugaidi eneo la Sahel

Mkutano wa kilele wa G5 Sahel huko Nouakchott, Juni 30, 2020.
Mkutano wa kilele wa G5 Sahel huko Nouakchott, Juni 30, 2020. Ludovic Marin /Pool via REUTERS

Viongozi wa nchi za G5 Sahel na washirika wao wa kimataifa ambao walikutana huko Nouakchott Jumanne hii, Juni 30 wameonyesha nia yao ya kuimarisha maendeleo yaliyopatiakana katika vita dhidi ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha katika miezi ya hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi walioshiriki mkutano wa Nouakchott, nchini Niger, wamekaribisha kwanza maendeleo yaliyopatikana kwa kipindi cha miezi sita iliyopita: kuongeza nguvu kikosi cha Ufaransa cha Barkhane, mafanikio ya kijeshi katika eneo la mipaka 3, maboresho ndani ya kikosi cha G5 Sahel tangu kuanzishwa kwa makao makuu ya pamoja. "Juhudi zinaendelea, maendeleo yanaonekana, lakini bado hayatoshi," amekiri Mohamed Ould Ghazouani.

"Mkutano huu wa Nouakchott umetupatia fursa ya kubadilishana maoni juu ya mabadiliko ya hali ya usalama katika eneo hili. Kwa kweli sio tu kuongezeka kwa machafuko nchini Libya na athari zake mbaya kwa ukanda wote, lakini pia hatari ya kutanuka kwa makundi ya kigaidi katika maeneo mapya. Aamezungumzia shambulio la Kafolo Kaskazini mwa Côte d'Ivoire Juni 11, ambapo ameonyesha hofu ya wanajihadi hao kutoka maeneo ambayo wamepigo, kuelekea nchi za pwani.

Wakati huo huo Ghazouani ameomba nchi masikini zifutiwe mzigo wa madini.

Mara baada ya mkutano huo uliolenga kutathmini mkakati mpya katika mapambano na makundi ya kigaidi, Rais Macron alisema kumekuwa na matokeo ya kushangaza kama vile kuyachukua maeneo kutoka mikononi mwa makundi ya kigaidi.

Mkutano huo uliitishwa ili kuimarisha mbinu za kimkakati, zilizochochewa na mfululizo wa mashambulizi ya mwaka jana yaliyosababisha askari 13 wa Ufaransa kuuawa katika ajali ya helkopita. Chini ya mabadiliko hayo, Ufaransa iliongeza idadi ya askari 500 katika kikosi chake cha Barkhane cha kupambana na ugaidi ukanda wa Sahel, na kufanya jumla ya askari wake kufikia 5,100. Tangu wakati huo wanajihadi wameendeleza mashambulizi ya karibu kila siku, lakini pia walimpoteza kiongozi muhimu kwenye uvamizi wa vikosi vya Ufaransa na pia mapigano ya ndani.