AFRIKA KUSINI-CORONA-AFYA

Afrika Kusini yafanya jaribio la kwanza la chanjo ya Covid-19

Afrika Kusini imeanza jaribio la kwanza la kliniki la chanjo ya Covid-19 barani Afrika. Chanjo hii iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na tayari imeanza kufanyiwa majaribio kwa binadamu nchini Uingereza.

Chanjo inayoitwa ChAdOx1 nCoV-19 inatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa watu 2000 waliojitolea nchini Afrika Kusini.
Chanjo inayoitwa ChAdOx1 nCoV-19 inatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa watu 2000 waliojitolea nchini Afrika Kusini. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Afrika Kusini inakaribia kufikisha kesi 140,000 za maambukizi ya Corona na watu 2,500 wamefariki dunia na bado ni nchi iliyoathiriwa zaidi barani Afrika na janga hili la Covid-19.

Chanjo inayoitwa ChAdOx1 nCoV-19 inatarajiwa kufanyiwa majaribio kwa watu 2000 waliojitolea nchini Afrika Kusini. Vipimo vya kliniki vinaendelea nchini Uingereza kwa watu 4,000. Na utafiti mwingine umepangwa nchini Brazil kwa watu 5,000.

Lengo ni kujua ikiwa chanjo hii ni nzuri katika maeneo tofauti ya dunia na kwa idadi kubwa ya watu. Watafiti pia wanataka kujua ikiwa watu walioambukizwa virusi vya UKIMWI wanaweza pia kulindwa. Nchini Afrika Kusini, zoezi hilo litahusisha watu 50 walioambukizwa virusi vya UKIMWI.

Mwezi Aprili mwaka jana, wanasayansi wawili kutoka Ufaransa walizungumza kwenye runinga juu ya uwezekano wa kutumia Afrika kama "eneo la jaribio" kwa chanjo. kauli hiyo ilizua hali ya sintofahamu. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus, alilaani kauli hiyo akisema ni ya "ubaguzi wa rangi" na ya "urithi wa fikra za kikoloni".

Mbali na uhasama huo, viongozi wa Afrika Kusini wamejitolea kushiriki katika utafiti huu, wakisema kwamba bara la Afrika halipaswi kutengwa na utafiti wa kisayansi duniani.

"Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya Corona huongezeka kila siku, amesema Dk Sandile Buthelezi, Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya, huku akibaini kwamba maendeleo ya chanjo ndio suluhisho pekee kwa muda mrefu na tunaunga mkono kikamilifu 'timu inayofanya jaribio hili".

Na Profesa Madhi ameongeza akisema kwamba "ni muhimu kuwa na data ya kisayansi kwa muktadha wa Kiafrika ikiwa tunataka Waafrika waweze kufaidika na chanjo katika siku za usoni."

Zaidi ya chanjo 200 za Corona zinafanyiwa utafiti duniani kote, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), majaribio ya kliniki kwa binadamu kadhaa yanaendelea.