G5 SAHEL-UFARANSA-HAKI-USALAMA

G5 Sahel: Suala la mauaji dhidi ya raia laibua maswali mengi katika eneo la Sahel

Katika mkutano wa kilele wa G5 Sahel (Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad) pamoja na Ufaransa huko Nouakchott Jumanne wiki hii, wakuu wa nchi walijadili swali la mauaji dhidi ya raia.

Wanajeshi wa Mali, askari wa kikosi cha pamoja cha G5 Sahel, wakipiga doria karibu na mpaka na Burkina Faso. (picha ya kumbukumbu)
Wanajeshi wa Mali, askari wa kikosi cha pamoja cha G5 Sahel, wakipiga doria karibu na mpaka na Burkina Faso. (picha ya kumbukumbu) Daphné BENOIT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitangaza kwamba "jamii ya Fulani sio adui wa mtu".

Maneno hayo ya rais wa Ufaransa yamekaribishwa na mashirika mbalimbali ya kiraia nchini Burkina Faso. Kulingana na shirika moja nchi humo, hii ni hatua ya kwanza katika vita dhidi ya ugaidi na ulinzi wa raia ambayo imepata nafasi muhimu kwa kuweza kuzingatiwa na vitendo viovu kukomeshwa.

Daouda Diallo, msemaji wa muungano wa mashirika ya kiraia wa KISAL nchini Burkina Faso, mashirika yanayotetea haki ya jamii ya kuhamahama na jami ya walio wachache, amempongeza Rais Macron "kwa kwa kulipa nafasi suala hilo la mauaji dhidi ya raia ambalo limekuwa sugu na kukosa suluhu katika Ukanda aw Sahel", lakini ametoa wito kwa rais wa Ufaransa" kutia katika vitendo aliyoyasema".

"Kwetu sisi, mkakati uliotumiwa kwa sasa sio mzuri kwa kuhakikisha usalama wa raia wa Burkina Faso. Mkakati sio lazima uwe tu wa kijeshi, lazima pia kuwe na mipango ya mazungumzo na wadau wote wakuu, nikimaanisha jamii kubwa nchini Burkina Faso. Inabidi kuwepo na mpano wa kitaifa juu ya maswala ya jamii ili kuziweka jamii pamoja, kuwepo na mshikamano baina ya jamii ili kufanikiwa vyema katika vita hivi dhidi ya ugaidi, " ameongeza Daouda Diallo.

Nchini Mauritania pia, mashirika ya kiraia yametoa wito wa kulinda vilivyo raia baada ya kauli hii ya raisa aw Ufaransa.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliyofanyika baada ya mkutano huo wa Nouakchott, mbunge na kiongozi wa shirika linalopiga vita unyanyasaji IRA, Biram Dah Abeid, alitoa wito kwa Rais Emmanuel Macron kuweka shinikizo kwa marais wa nchi za Ukanda wa Sahel, ili mauaji hayo yanayotekelezwa na majeshi ya G5 Sahel dhidi ya raia wa Jamii ya Fulani yakomeshwe mara moja.