DRC-CENI-SIASA

DRC: Uteuzi wa Ronsard Malonda kama mwenyekiti wa CENI wazua mvutano

Rais mpya wa CENI anapingwa na vyama vingi vya kisiasa kama UDPS na Lamuka.
Rais mpya wa CENI anapingwa na vyama vingi vya kisiasa kama UDPS na Lamuka. Caroline Thirion / AFP

Hatua ya Bunge la taifa nchini DRC kumteua Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (CENI) inaendelea kuzua mvutano nchini DRC. Baada ya Kanisa Katoliki, Protestanti na Kimbungu, chama cha UDPS kimetoa msimamo wake kikisema kuwa hakikubaliani na uteuzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha UDPS kinashtumu mshirika wake madarakani FCC kusababisha hali hiyo, kwa kwa kujivunia wingi wa viti katika Bunge.

Kufuatia uteuzi huu mungano madaraki (CASH na FCC) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umegawanika. Chama cha UDPS kimefutilia mbali uteuzi wa Ronsard Malond kama mwenyekiti wa Ceni, kikisema kuwa "utaratibu uliotumiwa na FCC kumteua mgombea wake katika nafasi ya asasi za kiraia ni wa aibu".

Kwa upande wa chama hicho cha rais, mshirika wake madarakani hutumia "mabavu" kwa kutaka kuvunja sheria kwa mambo ambayo yanahitaji makubaliano ya kitaifa.

"UDPS inabaini kuwa Bwana Ronsard Malonda amekataliwa na kanisa Katolika, Protestani na Kimbangu ambayo inasemekana ndio yaliyomteuwa."

Wakati huo huo Chama cha UDPS kimeitisha maandamano makubwa ya amani siku ya Alhamisi wiki ijayo. Maandamano ambayo yatafanyika kwa kuzingatia hatua za kudhibiti maambukizi ya Covid-19, amesema Simon Kalenga msemaji wa chama cha UDPS.