ALGERIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yakabidhi Algeria mabaki ya miili 24 ya wapiganaji waliouawa wakati wa ukoloni

Picha za televisheni ya Algeria zinazoonyesha mabaki ya wapiganaji wa Algeria waliouawa wakati wa ukoloni yaliwasili Algiers, Julai 3, 2020.
Picha za televisheni ya Algeria zinazoonyesha mabaki ya wapiganaji wa Algeria waliouawa wakati wa ukoloni yaliwasili Algiers, Julai 3, 2020. Roy ISSA / AFP / Algerian TV

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, mwenyewe ndiye alipokea fuvu 24 za raia wa Algeria waliouawa walipokuwa wakipigana katika vita mwanzoni mwa kipindi cha ukoloni wa Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Miili ya wahanga hao wa Algeria ilipokelewa jana Ijumaa, Julai 3, kwenye Jumba la Utamaduni la Algiers.

Mabaki hayo yaliwasili nchini Algeria jana mchana baada ya kurejeshwa na Ufaransa kufuatia ombi rasmi lililotolewa na viongozi wa Algeria mwaka wa 2018.

Mabaki hayo, ikiwa ni pamoja na fuvu - za viongozi 24 na wapiganaji wenzao ambao walipambana dhidi ya jeshi la Ufaransa kwa kutafuta uhuru yalisafirishwa na ndege ya kijeshi ya Ufaransa hadi nchini Algeria.

Wahanga hao waliuawa mwanzoni mwa karne ya 19 na askari wa Ufaransa ambao walikuja kutawala nchi yao. Walipigana kwa nguvu zao kutetea uhuru wa Algeria.

Kati ya myaka wa 1838 na 1865, vita dhidi ya udhibitii wa Ufaransa ilisababisha vifo vingi kwa upande wa Algeria. Wapiganaji jasiri waliuawa kwa kupigwa risasi na wakoloni, kisha miili yao miili yao kukatwa kwa kulipiza kisasi.

Algeria ilipata uhuru kutoka mikononi mwa utawala wa Kikoloni wa Ufaransa Julai 3, 1962.