MALI-USALAMA

Wanajeshi tisa wa Mali wauawa katika shambulio la kushtukiza

Askari wa Mali wanapiga doria, wakimtafuta adui.
Askari wa Mali wanapiga doria, wakimtafuta adui. © Serge Daniel/RFI

Hali ya usalama nchini Mali bado ni tete, wakati makundi ya watu wenye silaha yanaendelea kutekeleza mashambulizi ya hapa na pale dhidi ya raia. Katika mashambulizi hayo pia viksi vya ulinzi na usalama vinalengwa.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mashahidi wanajeshi wasiopungua tisa wameuawa hivi punde katikati nchini Mali, huku wengine wakijeruhiwa.

Msemaji wa jeshi la Mali ameliambia shirika lahabari la AFP kwamba wanajeshi tisa wa Mali waliuawa katika shambulio la Alhamisi wakati walikuwa wamekwenda katika maeneo ambayo karibu watu thelathini waliuawa siku ya Jumatano katikati mwa nchi.

Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha wameuawa watu 30 katika vijiji kadhaa katikati ya nchi ya Mali, vyanzo vya usalama vimebaini.

Ripoti za maafisa wa serikali katika jimbo la Bankass wamesema mashambulizi hayo yalitokea siku ya Jumatano lakini haikuwa rahisi kupata taarifa hizo kutokana na ugumu wa kufika katika eneo la tukio.

Hakuna kundi lolote lililolaumiwa kuhusika na mauaji hayo katika eneo ambalo limeendelea kushuhudua uwepo wa makundi ya kijihadi na mapigano ya kikabila.