MALI-SIASA-USALAMA

Maamdamano ya kumtaka rais wa Boubacar Keita kujiuzulu yaendelea Mali

Upinzani waendelea na maandamano ya kutaka rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ajiuzulu, kutokana na mzozo wa kisiasa na utovu wa usalama.
Upinzani waendelea na maandamano ya kutaka rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ajiuzulu, kutokana na mzozo wa kisiasa na utovu wa usalama. RFI/Coralie Pierret

Maandamano zaidi yameshuhudiwa nchini Mali kumshinikiza Rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita, kujiuzulu kutokana na mzozo wa kisiasa na utovu wa usalama.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa vyama vya upinzani, pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Mali, wamefahamisha kuwa waliitisha maandamano hayo baada ya kukutana na rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubakar Keita, IBK kwa mazungumzo ambayo hayakuzaa matunda kufuatia kile wanachokisema serikali ya Bamako haina mpango mkakati wa kuyatokomeza makundi ya wapiganaji wa kigaidi wanaoendeleza mashambulizi yao eneo la kasakzini mwa taifa hilo.

Maelfu ya watu waliitikia wito wa kuandamana wakiwa na mabango yenye maandishi ya kuikashifu serikali ya Mali, huku wapinzani wakimtaka rais IBK kuhakikisha usalama unarejeshwa katika maeneo kadhaa yanayodhibitiwa na wapiganaji wa kijihadi. Maelfu ya watu walilazimika kutoroka makazi yao tangu 2012.

Keita, ambaye amekuwa madarakani tangu 2013, ameshindwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwaka 2012 kuwa ataimarisha usalama wa nchi hiyo.

Video iliyotumwa kwenye akaunti ya Twitter ya rais siku ya Jumapili ilionesha mkutano kati ya rais na Mahmoud Dicko, imamu na sura ya kikundi kinachojulikana kama Juni 5, katika mji mkuu Bamako siku ya Jumamosi.