DRC-ITURI-CODECO-USALAMA

Serikali ya DRC yatoa wito kwa kundi la CODECO kujiunga na mchakato wa amani

Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006.
Askari wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 14, 2006. REUTERS

Rais wa DRC Félix Tshisekedi ametuma ujumbe wa waliokuwa waasi wa zamani jimboni Ituri miongoni mwao kiongozi wa Kundi la wapiganaji wa FNI Floribert Njabu, kuwahamasisha wapiganaji wa CODECO kukubali kuweka silaha chini,na kuacha kuuwa watu huko Djugu, mkoani Ituri, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa viongozi wa zamani wa waasi, maafisa kutoka Ituri, waliwasili wiki hii katika mkoa huo ili kuanzisha mara moja mchakato huo.

Haya yanajiri siku moja baada ya kuuawa kwa watu 11 wakiwemo wanajeshi, polisi na afisa wa serikali baada ya msafara wao kushambuliwa na waasi katika kijiji cha Matete, wilayani Djugu mwishoni mwa juma lililopita.

Mapema wiki iliyopita Ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (UNJHRO) iliripoti kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo la Ituri.

Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka nchini DRC, askari wengi wametumwa kusaidi vikosi vingine vinavyosimamia amani katika mkoa huo unaoendelea kukumbwa na vitisho mbalimbali.

Hivi karbuni kamati ya ulinzi ya Bunge iliiagiza serikali kuimarisha uwezo wa majeshi ya FARDC kwa kuunda kitengo maalum kitakachohusika na ulinzi wa mipaka.

Katika eneo la Irumu, operesheni za pamoja zimekuwa zinaendeshwa na askari walio katika mkoa jirani wa Kivu Kaskazini tangu wiki iliyopita, kwa lengo la kupambana na kundi la wanamgambo wa Maï-Maï. Mkoa wa Ituri unakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mara kwa mara wa wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda la ADF kutoka wilaya ya Beni, Mashambulizi ya hapa na pale ya kundi la wanamgambo wa CODECO dhidi ya raia.