MALI-SIASA-USALAMA

Mgogoro wa kisiasa Mali: Washirika wa Rais IBK, watoa wito kwa mazungumzo

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta Desemba 13, 2017
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta Desemba 13, 2017 LUDOVIC MARIN / AFP

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (IBK) anaendelea kukutana na wadau mbalimbali ili kupata suluhisho la mzozo wa kisiasa ulioibuka kwa kupinga uchaguzi wa wabunge uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Rais IBK tayari amewapokea wawkilishi wa upinzani tangu siku ya Jumapili. Hata hivyo kutokana na kuwa upinzani haukurudhika na mazungumzo hayo, umerudi kuomba kwa rais Ibrahim Boubacar Keita ajiuzulu.

Siku ya Jumatatu, muungano wa vyama vya kisiasa na mashirika mbalimbali yanayomuunga mkono rais IBK (CFR), wamelaani madai ya upinzani na kutoa wito kwa mazungumzo.

"Tunasema kwamba ombi la vyama vya upinzani na washirika wao (M5) sio halali, halina msingi na halifai, kwa sababu halizingatii mantiki yoyote ya uchaguzi, wala sheria za Jamhuri. Tunawatolea wito pia kuwa na huruma na taifa lao kwa kukubali kuketi kwenye meza ya mazungumzo, kwa kuliendeleza taifa letu, " amesema Fatoumata Sacko, naibu Mratibu wa CFR.

Rais Keita, ambaye amekuwa madarakani tangu 2013, ameshindwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais mwishoni mwa mwaka 2012 kuwa ataimarisha usalama wa nchi hiyo.