SOMALIA-UCHAGUZI-USALAMA-SIASA

Upinzani wapinga hatua ya kusogeza mbele uchaguzi Somalia

Miongo mitatu, tangu kuanza kwa vita vinavyoendelea vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia, machafuko pamoja na ugaidi ni mambo yaliyokita mizizi katika mzozo wa kisiasa tangu uhuru wa nchi hiyo.
Miongo mitatu, tangu kuanza kwa vita vinavyoendelea vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia, machafuko pamoja na ugaidi ni mambo yaliyokita mizizi katika mzozo wa kisiasa tangu uhuru wa nchi hiyo. STUART PRICE / AU-UN IST PHOTO / AFP

Vyama vya upinzani nchini Somalia vinapinga hatua ya Tume ya Uchaguzi kuahirisha Uchaguzi Mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka huu kwa hofu kuwa hatua hiyo itasababisha mapigano kati ya koo mbalimbali nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Vyanzo kadhaa kutoka Somalia vimebaini kwamba Tume ya Uchaguzi nchini Somalia imeahirisha kwa miezi 13 uchaguzi wa bunge na urais uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu, kutokana na matatizo ya kiusalama nchini humo.

Wiki iliyopita Somalia iliadhimisha  miaka 60 ya uhuru, ikiwa miongoni mwa mataifa ya Afrika Mashariki kuanza kujitawala, lakini raia wake wameendelea kuishi kwa shida huku wengi wakikimbilia katika nchi jirani ya Kenya

Miongo mitatu, tangu kuanza kwa vita vinavyoendelea vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, machafuko pamoja na ugaidi ni mambo yaliyokita mizizi katika mzozo wa kisiasa tangu uhuru wa nchi hiyo.