DRC-MAUAJI-USALAMA

Watu 800 wauawa Mashariki mwa DRC

Kijiji cha Manzalawu (Manzalaho) katika eneo la Beni, mnamo Februari 18, 2020, baada ya shambulio lililoendeshwa na waasi wa ADF. Karibu watu 15 waliuawa katika kijiji hiki chenye wenyeji 1000 ambao wengi wao walilazimika kutoroka makazi yao.
Kijiji cha Manzalawu (Manzalaho) katika eneo la Beni, mnamo Februari 18, 2020, baada ya shambulio lililoendeshwa na waasi wa ADF. Karibu watu 15 waliuawa katika kijiji hiki chenye wenyeji 1000 ambao wengi wao walilazimika kutoroka makazi yao. Alexis Huguet / AFP

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inoshughulikia Haki za binadamu katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema aaia wasiopungua 800 wameuawa na wapiganaji waasi wenye silaha wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) mashariki mwa DRC tangu Januari 2019.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa jana Jumatatu, imelaani mauaji yanayoendelea huko mashariki mwa Congo na kusema kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Wiki iliyopita serikali ya DRC imetoa wito kwa kundi la CODECO kujiunga na mchakato wa amani.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi alituma ujumbe wa waliokuwa waasi wa zamani jimboni Ituri miongoni mwao kiongozi wa Kundi la wapiganaji wa FNI Floribert Njabu, kuwahamasisha wapiganaji wa CODECO kukubali kuweka silaha chini,na kuacha kuuwa watu huko Djugu, mkoani Ituri, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Hivi karbuni kamati ya ulinzi ya Bunge iliiagiza serikali kuimarisha uwezo wa majeshi ya FARDC kwa kuunda kitengo maalum kitakachohusika na ulinzi wa mipaka.

Mapema wiki iliyopita Ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (UNJHRO) iliripoti kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika jimbo la Ituri.

Mkoa wa Ituri unakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mara kwa mara wa wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda la ADF kutoka wilaya ya Beni, Mashambulizi ya hapa na pale ya kundi la wanamgambo wa CODECO dhidi ya raia.