BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Zaidi ya kumi waangamia katika mashambulizi Kaskazini mwa Burkina Faso

Askari wa Burkina Faso wakiwa katika mazoezi.
Askari wa Burkina Faso wakiwa katika mazoezi. MICHELE CATTANI / AFP

Watu wasiopungua kumi wameuawa katika mashambulizi mawili yaliyotekelezwa na watu waliojihami kwa bunduki katika Jimbo la Kati Kaskazini nchini Nigeria.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yaliyotokea Jumatatu wiki hii yaligharimu maisha ya watu wengi ikiwa ni pamoja na meya wa wilaya ya Pensa / Baaalogho, ambaye aliuawa katika shambulio la kwanza. Askari wawili pia ni miongoni mwa watu waliouawa.

Meya huyo anakuwa kiongozi wa pili ambaye anauawa katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na makundi ya kigaidi nchini Burkina Faso, baada ya mauaji ya meya wa wilaya ya Djibo, mwezi Novemba 2019.

Shambulio hilo lililogharimu maisha ya meya wa wilaya ya Pensa / Baaalogho lilitokea kilomita 30 kutoka mji wa Baaalogho. Walinzi wake wawili walijeruhiwa.

Burkina Faso imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya makundi ya watu wenye silaha, ikiwa ni pamoja na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu, yanayohatarisha usalama katika nchi za ukanda wa Sahel.