BURKINA FASO_HRW-HAKI

HRW yavinyooshea kidole cha lawama vikosi vya usalama nchini Burkina Faso

Wanajeshi wa Burkina Faso wakati wa mazoezi ya kupambana na ugaidi mashariki mwa nchi, Aprili 13, 2018. (Picha kumbukumbu)
Wanajeshi wa Burkina Faso wakati wa mazoezi ya kupambana na ugaidi mashariki mwa nchi, Aprili 13, 2018. (Picha kumbukumbu) AFP PHOTO/ISSOUF SANOGO

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Right Watch limeendelea kuvishtumu vikisi vya usalama vya Burkina Faso kuhusuika na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyotolewa leo Jumatano asubuhi kuhusiana na uchunguzi juu ya uwepo wa makaburi ya halaiki huko Djibo katika Jimbo la Sahel nchini Burkina Faso, miili 180 imedunduliwa. Kulingana na uchunguzi huo, miili ya watu ilitelekezwa kati ya mwezi Novemba 2019 na Juni 2020 karibu na eneo la Djibo. Kulingana na HRW, ushahidi unaonyesha kuwa vikosi vya usalama vya serikali vilihusika katika mauaji hayo ya kikatili.

"Ripoti yetu inaonyesha uwepo wa makaburi ya halaiki huko Djibo, kaskazini mwa Burkina Faso ambapo miili 180 ya wanaume iligundiliwa. Na ushahidi tuliokusanya wakati wa uchunguzi wetu unaonyesha kwamba vikosi vya usalama vya serikali vilihusika katika mauaji ya kikatili ya watu wengi. Wakazi wa eneo la Djibo, ambao waliona miili hiyo na ambao tuliwahoji wakati wa uchunguzi wetu, walibaini kwamba watu wote hao waliouawa walikuwa wanaume, wengi wao kutoka jamii ya Fulanii, na kulingana na wakazi hao, wengi wa watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi kwani walipatikana wakiwa wamefunikwa nyuso za kwa kitambaa , huku mikono pia ikifungwa. Hapa tunaridhishwa na hatua ya serikali baada ya ripoti, kwamba serikali imeazimia kufanya uchunguzi, lakini hii sio mara ya kwanza serikali kuahidi kufanya hivyo. Tunatoa wito kwa serikali kuweka ahadi zake katika vitendo, na ifanye uchunguzi kuhusu suala hilo na sheria ifuate mkondo wake kwa wahusika, " amesema Bénédicte Jeannerod, Mkurugenzi wa HRW nchini Ufaransa katika mahojiano na Kpénahi Traoré.