COTE D'IVOIRE-COULIBALY-USALAMA-SIASA

Cote d’Ivoire yaomboleza kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly

Katibu mkuu wa zamani wa ikulu ya rais nchini Cote d'Ivoire, Amadou Gon Coulibaly ambaye aliteuliwa kama Waziri Mkuu na Rais Alassane Ouattara, Januari 10, 2017.
Katibu mkuu wa zamani wa ikulu ya rais nchini Cote d'Ivoire, Amadou Gon Coulibaly ambaye aliteuliwa kama Waziri Mkuu na Rais Alassane Ouattara, Januari 10, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon

Cote d’Ivoire inaomboleza kifo cha cha Waziri Mkuu wa Cote d’Ivoire, Amadou Gon Coulibaly, aliyefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Alhamisi akiwa na umri wa miaka 61.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 alikuwa amechaguliwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, baada ya Alassane Ouattara kusema kuwa hatowania muhula wa tatu.

Rais wa Cote d’Ivoire Alassane Ouattara jana usiku alitangaza kwamba nchi yake imeingia kwenye msiba wa kuondokewa ghafla na Coulibaly ambaye alimteua kuwa mrithi wake katika uchaguzi unaopangwa kufanyika nchini humo mwezi Oktoba mwaka huu.

Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly alishiriki kwenye kikao cha kila wiki cha Baraza la Mawaziri cha serikali ya Cote d’Ivoire, ghafla hali yake ikawa mbaya na amefariki dunia akipewa matibabu hospitalini.

Bwana Coulibali alifanyiwa upandikizaji wa moyo 2012 na alikuwa ameelekea Ufaransa tarehe 2 Mei ili kuwekewa bomba katika mshipa wake wa damu.

“Nimerudi kuchukua mahala pangu kando ya rais , ili kuendelea na jukumu la kujenga taifa letu”, Amadou Gon Coulibaly alisema aliporudi Alhamisi iliopita.