Maandamano ya aina yoyote yapigwa marufuku DRC
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani Gilbert Kankonde imepiga marufuku maandamano yote yaliyotarajiwa kuanza leo kupinga uteuzi wa Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya uchaguzi CENI nchini humo.
Imechapishwa:
Chama cha UDPS cha rais Felix Thisekedi kilikuwa kimepanga maandamano yake hivi leo, huku muungano wa upinzani wa Lamuka ukiitisha maandamano Jumatatu ya Julai 13, na kufuatiwa na maandamano yaliyoandaliwa na Kamati ya Walei wa Kanisa Katoliki CLC tarehe 19 mwezi huu.
Hatua ya Bunge la taifa nchini DRC kumteua Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (CENI) inaendelea kuzua mvutano nchini DRC.
Chama cha UDPS kinashtumu mshirika wake madarakani FCC kusababisha hali hiyo, kwa kwa kujivunia wingi wa viti katika Bunge.
Kufuatia uteuzi huu mungano madaraki (CASH na FCC) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umegawanika. Chama cha UDPS kimefutilia mbali uteuzi wa Ronsard Malond kama mwenyekiti wa Ceni, kikisema kuwa "utaratibu uliotumiwa na FCC kumteua mgombea wake katika nafasi ya asasi za kiraia ni wa aibu".
Kwa upande wa chama hicho cha rais, mshirika wake madarakani hutumia "mabavu" kwa kutaka kuvunja sheria kwa mambo ambayo yanahitaji makubaliano ya kitaifa.