NIGERIA-MAUAJI-USALAMA

Askari thelathini na tano wauawa katika shambulio Nigeria

Makundi yenye silaha yakiongozwa na Boko Haram kwa zaidi ya miaka 10 yamesababisha ukosefu wa usalama Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifi vay watu Elfu 36 na zaidi ya Milioni mbili kuyakimbia makwao.
Makundi yenye silaha yakiongozwa na Boko Haram kwa zaidi ya miaka 10 yamesababisha ukosefu wa usalama Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifi vay watu Elfu 36 na zaidi ya Milioni mbili kuyakimbia makwao. premiumtimesng

Idadi ya wanajeshi wa Nigeria waliouawa baada ya kushambuliwa na wanajihadi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, imeongezeka kutoka 23 na kufikia 35.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wanasema pamoja na vifo hivyo, wanajeshi wengine 30 bado hawajapatikana.

Wapiganaji wanaojihusisha kwa karibu na kundi la Islamic State, walitekeleza shambulizi la kushtukiza dhidi ya msafara wa wanajeshi hao katika kijii cha Bulabulin siku ya Jumanne katika Jimbo la Borno.

Awali, wanajeshi 23 ndio waliokuwa wameripotiwa kupoteza maisha katika shambulio dhidi ya wanajeshi hao, na baadaye kubainika kuwa wengine walikuwa wametoweka.

Afisa wa kijeshi ameliambia shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, wanajeshi 35 wameuwa, 18 wamejeruhiwa na wengine 30 hawajulikani walipo.

Makundi yenye silaha yakiongozwa na Boko Haram kwa zaidi ya miaka 10 yamesababisha ukosefu wa usalama Kaskazini mwa Nigeria na kusababisha vifo vya watu Elfu 36 na zaidi ya Milioni mbili kuyakimbia makwao.