COTE D'IVOIRE-COULIBALY-USALAMA-SIASA

Mrithi wa Ouattara atafutwa kwa udi na uvumba Cote d'Ivoire

Rais Ouattara alitangaza mnamo mwezi Machi kuwa hatowania tena urais baada ya miaka 10 ofisini na tayari alikuwa amemteua Coulibaly kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu.
Rais Ouattara alitangaza mnamo mwezi Machi kuwa hatowania tena urais baada ya miaka 10 ofisini na tayari alikuwa amemteua Coulibaly kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu. ISSOUF SANOGO / AFP

Siku moja baada ya kifo cha aliyekuwa waziri Mkuu wa nchi ya Cote d’Ivoire Amadou Gon Coulibaly tayari kumeibuka sintofahamu kuhusu nani atamrithi rais wa nchi Alassane Ouattara, wakati wa uchaguzi wa urais wa Oktoba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Ni majuma kadhaa tu yamepita tangu chama tawala cha rais Ouattara kumteua Coulibaly kuogombea kiti cha urais kwenye uchaguzi huo.

Chama tawala sasa kinazo siku chache tu kumteua mgombea mwingine atakayepeperusha bendera ya chama tawala cha RHDP.

Kulingana na vyanzo kadhaa nchini Cote d'Ivoire, viongozi wa chama cha RHDP wamekubaliana kumshinikiza Rais Alassane Outtara kuwania muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi wa mwezi Oktoba baada ya kifo cha waziri mkuu Amadou Coulibaly.

Hata hivyo Rais Ouattara alitangaza mnamo mwezi Machi kuwa hatowania tena urais baada ya miaka 10 ofisini na tayari alikuwa amemteua Coulibaly kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu.

Muda wa mwisho wa kuwasilisha jina la mgombea wa urais ni Julai 31.