BURKINA FASO-SIASA

Burkina: Vyama vya siasa vyapinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge

Wabunge wa Burkina Faso wamependekeza kuahirisha uchaguzi wa wabunge kwa sababu ya ukosefu wa usalama (picha ya kumbukumbu)
Wabunge wa Burkina Faso wamependekeza kuahirisha uchaguzi wa wabunge kwa sababu ya ukosefu wa usalama (picha ya kumbukumbu) ISSOUF SANOGO / AFP

Vyama vya siasa nchini Burkina Faso vimefutilia mbali pendekezo la wabunge kuahirisha uchaguzi wa wabunge hadi mwisho wa mwaka 2021.

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyotolewa Jumatano iliyopita kwa rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kaboré, wabunge walipendekeza kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge kwa sababu wakitoa sababu ya kudoroa kwa usalama katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Kwa mujibu wa wabunge, itakuwa vigumu kufanya uchaguzi katika mikoa kadhaa iliyoathiriwa na mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali.

Wakati huo huo walipendekeza uchaguzi wa urais na ule wa wabunge wa Novemba 22 ufanyike kwa hatua mbili: uchaguzi wa urais ufanyike kwa upande mmoja na ule wa wabunge kwa upande mwingine.

Lakini muungano wa vyama vya siasa vilivyo madarakani na vyama vya upinzani vimetaka kalenda ya uchaguzi iheshimishwe kwa kuzingatia hoja hiyo ya wabunge.

Rais wa Burkina Faso alituma nakala za ripoti ya wabunge kwa vyama mbali mbali vya siasa. Vyama vya siasa vilivyo madarakani na vile vya upinzani waliafikiana kuwa uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika kwa hatua mbili lakini kwa tarehe 22 Novemba 2020.