AFRIKA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya vya maambukizi vyaongezeka Afrika Kusini

Hivi karibuni Rais Cyril Ramaphosa aliwaonya raia wake kwamba serikali imetekeleza jukumu lake na sasa raia ndio wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu kujikinga na ugonjwa huo hatari.
Hivi karibuni Rais Cyril Ramaphosa aliwaonya raia wake kwamba serikali imetekeleza jukumu lake na sasa raia ndio wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu kujikinga na ugonjwa huo hatari. AFP/Rodger Bosch

Afrika Kusini imepitisha idadi ya watu 200,000 walioambukizwa virusi vya Corona wiki hii na inaendelea kukabiliwa na ongezeku kubwa la maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Afrika Kusini imefikisha idadi ya vifo 3 860 vinavyotokana na virusi vya Corona baada ya vifo vipya 140 katika muda wa saa 24 zilizopita. Hii ni idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo barani Afrika.

Kufikia sasa Afrika kusini imerekodi visa 251,000 vya maambukizi ya vitusi vya Corona, baada ya visa vipya 12, 288 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita. Wagonjwa 118 wamepona ugonjwa huo hatari.

Mkoa wa Gauteng, ambapo kunapatikana mji wa Johannesburg na mji mkuu wa Pretoria, ndio maeneo yanayoathirika zaidi na ugonjwa wa Covid-19.

Kulingana na mwandishi wetu huko Johannesburg, Noé Hochet-Bodin, Mkoa wa Gauteng ulirekodi kesi 28,000 za maambukizi ya virusi vya Corona wiki mbili zilizopita. Leo, wakazi 81,000 wameambukizwa virusi hivyo.

Taasisi ya kitaifa ya takwimu inaonya kuwa takwimu hizi zinatarajia kuongezeka mara tatu ndani ya siku 10 zijazo.

Hivi karibuni Afrika Kusini ilichukuwa hatua ya kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya Corona.

Maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi kama vile baa, vituo vya kibiashara, mikahawa vilifunguliwa tangu wiki mbili zilizopita.

Hivi karibuni Rais Cyril Ramaphosa aliwaonya raia wake kwamba serikali imetekeleza jukumu lake na sasa raia ndio wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu kujikinga na ugonjwa huo hatari.