AFRIKA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Afrika Kusini yachukua tena hatua kadha za kudhibiti maambukizi zaidi

Taasisi ya kitaifa ya takwimu inaonya kuwa takwimu hizi zinatarajia kuongezeka mara tatu ndani ya siku 10 zijazo.
Taasisi ya kitaifa ya takwimu inaonya kuwa takwimu hizi zinatarajia kuongezeka mara tatu ndani ya siku 10 zijazo. REUTERS/Mike Hutchings/File Photo

Afrika Kusini imerejesha tena masharti ya watu kutotembea na kuzuia uuzwaji wa pombe, baada ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona katika siku za hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya Laki Mbili na Elfu Sabini wameambukizwa virusi hivyo nchini humo na kulifanya taifa hilo kuwa na maambukizi makubwa barani Afrika, huku watu waliopoteza maisha, idadi ikifikia zaidi ya Elfu nne, na kuna wasiwasi kuwa huenda idadi ya vifo ikafika Elfu 50 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Taasisi ya kitaifa ya takwimu inaonya kuwa takwimu hizi zinatarajia kuongezeka mara tatu ndani ya siku 10 zijazo.

Hivi karibuni Afrika Kusini ilichukuwa hatua ya kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya Corona.

Maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi kama vile baa, vituo vya kibiashara, mikahawa vilifunguliwa tangu wiki mbili zilizopita.

Hivi karibuni Rais Cyril Ramaphosa aliwaonya raia wake kwamba serikali imetekeleza jukumu lake na sasa raia ndio wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu kujikinga na ugonjwa huo hatari.