CAR-UN-USALAMA

Askari wa Umoja wa Mataifa auawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji
Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji UN Photo/Nektarios Markogiannis

Askari mmoja wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Rwanda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MUNISCA) ameuawa katika shambulio la kushtukiza lililoendeshwa na kundi moja la wanamgambo Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Askari wengi wawili wamejeruhiwa shambulio hilo dhidi ya msafara wa magari ya kijeshi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (MUNISCA), Umoja wa Mataifa umetangaza katika taarifa.

Machafuko yanayoendelea kuikumba Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2013 ziliongezeka baada ya kusainiwa makubaliano ya amani kati ya serikali na vikosi kumi na nne vya makundi yenye silah mwezi Februari, 2019 , lakini mkataba wa usitishwaji mapigano haujatekelezwa vilivyo.

Katika taarifa yake, Umoja wa Mataifa umelinyooshea kidole cha lawama kundi lenye silaha la Retour (3R), moja ya makundi yaliyotia saini kwenye mkataba huo wa amani mwaka uliopita.