MALI-ICC-HAKI

Mali: Kesi ya mwanajihadi Al-Hassan yafunguliwa ICC

Al-Hassan anashtakiwa katika mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa eneo la Timbuktu lililopodhibitiwa na makundi ya waasi.
Al-Hassan anashtakiwa katika mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa eneo la Timbuktu lililopodhibitiwa na makundi ya waasi. EVA PLEVIER / ANP / AFP

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya jinai imefungua kesi ya Al-Hassan Ag Abdoul Aziz Ag Mohamed Ag Mahmoud mnamo leo Jumanne asubuhi.

Matangazo ya kibiashara

Mwanajihadi huyu anashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa eneo la Timbuktu lilipodhibitiwa na makundi ya Ansar Dine na Aqmi, mnamo mwaka 2012. Alikuwa mmoja wa maafisa wakuu wa polisi wanaohusika na masuala ya jamii.

Kulingana na mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda, Al-Hassan mwenyewe aliongoza doria inayohusika na kuchunguza raia na kuwataka waheshimu sheria za Kiislamu (Sharia'a). Inasemekana pia kuwa alishiriki katika utekelezaji wa maamuzi ya mahakama ya Kiislamu, akiwachapa viboko na adhabu zingine kali kwa wale walio na hatia.

Mwendesha mashtaka pia anamtuhumu kuwa alishiriki katika mfumo wa ndoa za kulazimishwa kati ya wapiganaji wa kijihadi na wanawake wa Timbuktu, sera ambayo ilisababisha visa kadhaa vya ubakaji wa mara kwa mara. Shutma ambazo zilifutuliwa mbali na upande wa utetezi wakati kesi hiyo iliposikilizwa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Julai 2019.

Kwa mujibu wa wakili wake, Al-Hassan sio "mwenye itikadi kali, muuaji, wala mwanajihadi".

Hata hivyo wakili wa Al-Hassan anaomba kesi hiyo ifungwe mara moja. Wakili Taylor amebaini kwamba Al-Hassan kutoka jamii ya Tuareg aliteswa na idara ya DST nchini Mali muda mfupi baada ya kukamatwa kwake mnamo mwaka 2017. Wakati huo, wachunguzi wa mwendesha mashtaka walikutana na kamishna huyo wa zamani wa polisi ya Kiislamu na kumuhoji, kabla ya kuomba waranti wa kukamatwa dhidi yake.