LIBYA-MAPIGANO-USALAMA

Libya: Kambi ya Haftar yaitaka Misri kuingilia kijeshi Libya

Bunge la Libya ambalo linamtambua Marshal Khalifa Haftar, linadai kuwa limevamliwa na wanajeshi wa Uturuki.
Bunge la Libya ambalo linamtambua Marshal Khalifa Haftar, linadai kuwa limevamliwa na wanajeshi wa Uturuki. REUTERS/Esam Omran Al-Fetori

Bunge llinalomuunga mkono Marshal Khalifa Haftar, lenye makao yake makuu mashariki mwa Libya, limelitolea wito rasmi jeshi la Misri kuingilia kijeshi Libya ikiwa kutatokea vitisho vya aina yoyote.

Matangazo ya kibiashara

Wiki chache zilizopita, Cairo ilitangaza nia yake ya kuingilia kati kwenye mzozo unaoendelea nchini Libya, huku ikishukizwa na namna vikosi vya serikali ya umoja wa kitaifa (GNA) visaidiwa na Uturuki, vinaendelea kusonga mbele katika uwanja wa vita.

"Tunatoa wito kwa vikosi vya jeshi la Wamisri kuingilia kati nchini Libya ili kulinda usalama wa kitaifa wa nchi hii na Misri, ikiwa wataona kuwa kuna tishio kwa usalama wa nchi zetu mbili," bunge la Libya lililochaguliwa mwaka 2014 limesema katika taarifa iliyolewa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii.

Bunge la Libya ambalo linamtambua Marshal Khalifa Haftar, linadai kuwa limevamliwa na wanajeshi wa Uturuki.

Akizungumza punde baada ya kukikagua kituo cha jeshi la wanamaji, kilichoko karibu na eneo la mpakani kati ya Misri na Libya katikati mwa mwezi uliopita, Rais wa Misri, Abdel Fattah al Sisi alisema kuwa nchi yake ina haki ya kuingilia moja kwa moja katika mzozo unaolikumba taifa jirani la Libya.

Hata hivyo jeshi la Tripoli kupitia msemaji wake, Mohammed Gununu, alisema “Libya haijawahi kutishia usalama wa nchi jirani, na kwamba wako tayari kujibu mashambulkizi yoyote kutoka nje ya taifa hilo”.

Uturuki inaiunga mkono serikali ya Tripoli inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.