DRC-UVIRA-USALAMA

Polisi yazima maandamano ya watu wenye hasira Uvira, DRC

Mafuriko katika mji wa Uvira, yalisababisha mamia ya wakazi kuhama makazi yao, Aprili, 2020.
Mafuriko katika mji wa Uvira, yalisababisha mamia ya wakazi kuhama makazi yao, Aprili, 2020. REUTERS/Crispin Kyalangalilwa

Polisi imekabiliana na waandamanaji wenye hasira ambao walikuwa wakilalamikia hali zao za maisha na mazingira ambamo wanaishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa miezi minne iliyopitaka katika mji wa Uvira mkoani wa kivu kusini.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji walitarajia kuanzia maandamano yao huko Kasenga na Kakombe ili kupeleka malalamiko yao hadi kwenye ofisi ya meya wa Uvira, lakini muda mfupi baadae, polisi iliingilia kati na kuzima maandamano hayo baada ay kutumia mabomu ya machozi.

Waandamanaji hao wana hofu kuwa huenda mvua zikarudi kunyesha kwa wingi, kabla hawajarejea katika nyumba zao.

“Nvua zitanyesha tena hivi karibuni baada ya miezi miwili, tutakimbilia wapi? Tuko tunapewa hifadhi hapa katika sehemu ya shule, hivi karibuni shughuli za masomo zitaanza . Sasa tutakuwa wageni wa nani?, “ amesema Bi Mamicho, mooja wa waandamanaji hao.

Shirika moja la kiraia huko Uvira linasema kuwa lina masikitiko kwa vile ahadi zote za misaada, na hasa ahadi ya serikali kutengeneza mifereji ya maji ili kuepuka mafuriko mapya haijatekelezwa.

André Bradunia, kiongozi wa shirika hilo, amelaani kitendo cha polisi kutumia nguvu kupita kiasi kwa kusambaratisha maandamano hayo.

“Polisi walitwambia kwamba tukifanya maandamano tutakiona cha mtima kuni. Matokeo nikwamba kuna watu wawili ambao wamefungwa, ” amesema André Bradunia.

Meya wa mji wa Uvira, Kiza Muhato, amesema kwamba hakupewa taarifa yoyote mapema kuhusu maandamano hayo, nakukumbusha kwamba maandamano hayaruhusiwe wakati huu serikali inapambana dhidi ya ugonjwa aw Covid-19.

Tangu mafuriko hayo mnamo miezi ya Machi na Aprili mwaka huu, serikali ya Kinshasa ilitoa msaada wa pesa za Congo Milioni Mia tatu, lakini pesa hizo hazitoshi kukidhi mahitaji ya watu zaidi ya Laki moja walioathirika na mafuriko hayo mjini Uvira.