ETHIOPIA-SUDANI-MSRI-NILE-USHIRILIANO

Ethiopia yaanza zoezi la kujaza maji bwawa la Grand Renaissance

Waziri wa maji wa Ethiopia, Seleshi Bekele, amesema ujazwaji maji wa bwawa hilo na ujenzi unafanyika pamoja na kusisitiza kuwa, kujaza bwawa hilo hakustahili kusubiri kumalizika ujenzi wa mradi huo.
Waziri wa maji wa Ethiopia, Seleshi Bekele, amesema ujazwaji maji wa bwawa hilo na ujenzi unafanyika pamoja na kusisitiza kuwa, kujaza bwawa hilo hakustahili kusubiri kumalizika ujenzi wa mradi huo. REUTERS/Tiksa Negeri

Ethiopia imeanza kujaza maji bwawa kubwa la kuzalisha umeme nchini humo,licha ya mazungumzo kati yake na Misri pamoja na Sudan kugonga mwamba kuhusu matumizi ya maji ya Mto Nile kufanikisha mradi huo.

Matangazo ya kibiashara

Ethiopia inasema kukamilika kwa mradi huo mkubwa barani Afrika, ni muhimu sana kwa mustakabili wa taifa hilo na utawaondoa mamilioni ya raia wake kutoka kwenye umasikini na kusambaza umeme barani Afrika.

Waziri wa maji nchini humo Seleshi Bekele amesema ujazwaji wa bwawa hilo na ujenzi unafanyika pamoja na kusisitiza kuwa, kujaza bwawa hilo hakustahili kusubiri kumalizika ujenzi wa mradi huo.

Hatua ya Ethiopia inakuja wakati ambapo nchi za Sudan na Misri zikitoa masharti mapya katika mazungumzo yaliyofanyika mapema wiki hii, yaliolenga kupata mwafaka kuhusu mzozo kati ya mataifa hayo matatu.

Hata hivyo, nchi ya Misri kupitia wizara ya mambo ya nje, imetaka kupewa maelezo na serikali ya Ethiopia kuhusu hatua hiyo, ikisema nchi hiyo itategemea asilimia 90 ya maji safi kutoka kwenye mto Nile na mradi huo unatishia uhai wa watu wake.

Mazungumzo ya kimataifa yakiongozwa na Marekani na Umoja wa Mataifa kujaribu kutatua mvutano huu, hayakufua dafu.