TUNISIA-SIASA-USALAMA

Waziri Mkuu wa Tunisia Elyes Fakhfakh aachia ngazi

Rais Kais Saied amesema hatua ya Elyes Fakhfakh (kwenye picha) kujiuzulu ni kuepusha migongano na taharuki katika taasisi za serikali katika taifa hilo.
Rais Kais Saied amesema hatua ya Elyes Fakhfakh (kwenye picha) kujiuzulu ni kuepusha migongano na taharuki katika taasisi za serikali katika taifa hilo. FETHI BELAID / AFP

Waziri Mkuu wa Tunisia Elyes Fakhfakh amejiuzulu, miezi mitano baada ya kuingia madarakani hatua ambayo inatishia mvutano wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Kaskazini, wakati huu linapoendelea kukabiliwa na changamoto za kiuchumi na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kwake kunakuja wakati huu chama cha Ennahdha, chenye idadi kubwa ya wabunge bungeni kuonekana kugawanyika kutokana na mgongano wa maslahi.

Rais Kais Saied amesema hatua ya Elyes Fakhfakh kujiuzulu ni kuepusha migongano na taharuki katika taasisi za serikali katika taifa hilo.

Tangu uchaguzi wa wabunge mwezi Oktoba mwaka ulipota, uhusiano kati ya Waziri Mkuu na uongozi wa chama hicho haujawa mzuri, suala ambalo wachambuzi wa siasa wanasema imechangia pakubwa kujiuzulu kwake.

Pamoja na kupata idadi kubwa ya viti bungeni, chama cha Ennahdha hakikupata idadi inayyohitajika ili kuunda serikali peke yake, na kulazimika kuingia kwenye muungano na vyama vingine ili kuunda serikali