CAR-UN-USALAMA-SIASA

UN yaonya kutokea kwa machafuko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, na mataifa jirani kuchukua hatua za kupambana na kile wanachokiita tishio la muda mrefu katika eneo hilo, hasa katika kipindi hiki miezi sita kabla ya uchaguzi wa rais.

Wanajeshi wa kigeni wakipiga doria katika mitaa ya Bria, mji unaokabiliwa na vitisho vya makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Picha ya kumbukumbu).
Wanajeshi wa kigeni wakipiga doria katika mitaa ya Bria, mji unaokabiliwa na vitisho vya makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. (Picha ya kumbukumbu). MIGUEL MEDINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti, kundi la wataalam wa UN wanaohusika na kuchunguza vikwazo vya silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati linabaini kurudiwa tena kwa mapigano, haswa Kaskazini Mashariki, yaliyochochewa na kuwasili kwa washambuliaji na silaha kutoka nje ya nchi kuja kuongeza nguvu makundi ya waasi

Hii imedhihirika baada ya kukutwa kwa vitambulusho vya wapiganaji maharufu raia wa mataifa ya Tchad na Sudan waliouawa ambao ni kutokana kundi liitwalo Kikosi cha Umma kwa ajili ya uzawa mpya wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati katika shambulio la Birao mwezi Februarimwaka huu. Au uwepo wa wanamgambo kadhaa wa jeshi la Misseriya la Sudan, miongoni mwa wapiganaji wa kundi hilo lenye silaha, wakati wa mapigano mwezi Machi.

Wataalam pia wanaona kuongezeka kwa mapigano kati ya wanamgambo wa kigeni kwenye ardhi ya Afrika ya Kati.

Jambo lingine linalotia shaka ni biashara ya kikanda ya silaha kutoka nchini Sudani, Chad, lakini pia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo mwezi April mwaka jana vilikamatwa vifaa vinavyotumiwa kwa kurusha mabomu na risase vikitokea mjini Gbadolite.

Mwishowe, wataalam wana wasiwasi juu ya kuendelea kujidhatiti kwa makundi yenye silaha  licha ya kwamba walisaini makubaliano ya kusitisha vita